Habari za Punde

CCM Z'bar Yajivunia Mafanikio ya Ziara ya Dk.SHEIN.

Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimewashukru na kuwapongeza Viongozi na wanachama wa Chama hicho walioshiriki na kufanikisha ziara ya Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein iliyofikia kilele chake jana.

Akitoa pongezi hizo kupitia taarifa kwa vyombo vya Habari, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar huko Afisini Kuu ya Chama  Kisiwa ndui Mjini hapa, alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa maendeleo ya CCM na nchi kwa ujumla.

Alisema kupitia ziara hiyo CCM imeweza kuongeza ari na hamasa kubwa kwa viongozo, watendaji na wafuasi wa Chama hicho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujipanga na uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Vuai alifafanua kwamba Chama hicho kina azna na rasilimali kubwa ya wananchi hasa wafuasi wa CCM wanaokiamini na kukipa ridhaa ya kushinda kwa kishindo kwa kila uchaguzi mkuu kutokana na utekelezaji wa Ilani za Uchaguzi za Chama hicho.


Alieleza kwamba pongezi hizo ni maalum kwa  viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi wa Mashina, Wenyeviti na Makatibu wa Matawi, Maskani, vinaja na Wazee waliojitokeza katika vikao vya Makamo mwenyekiti huyo kwa upande wa Mikoa yote Kichama Zanzibar.

Wengine ni watendaji wa CCM Afisi Kuu Zanzibar, Viongozi wa Chama na Serikali waliofuatana na Dkt. Shein katika ziara zake kichama zilizofanyika nchini.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kuwapongeza viongozi hao na wafuasi wa CCM kwa ujumla walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu pamoja na kuimarisha Chama.

“ Nawapongeza Viongozi wote walioshirikiana nasi katika ziara ya Makamo Mwenyekiti wetu Dkt. Shein, hakika mmetujengea imani na kutupa nguvu za kuendelea kusimamia maslahi ya chama chetu popote bila ya hofu.


Pia tumejifunza na kupata mambo mengi zikiwemo Changamoto na Mafanikio yaliyofanywa na CCM pamoja na Chama kwa muda mfupi toka serikali ya Dkt. Shein kuingia mdarakani.”, Alisema Vuai na kuongeza kuwa CCM ni chama cha watu wote wa rika na makundi tofauti na kitaendelea kulinda na kusimamia amani huku kikipinga vitendo vya ubaguzi na kuwagawa wananchi kwa itikadi zao.

Sambamba na Hayo aliwapongeza watu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika maandalizi ya ziara hiyo kuanzia mwano hadi kufikia kilele.

Katika ziara hiyo Dkt.Shein alipata fursa ya kuzungumza na Viongozi hao wakiwemo Mabalozi,  Wenyeviti na Makatibu wa Matawi wapatao 16,000 wa Wilaya 12 na Mikoa Sita (6) Kichama Unguja na Pemba.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.