Habari za Punde

Maofisa ZLSC, Mahakama na wa Waendesha Mashtaka Pemba Watembelea Magereza na Polisi Pemba.

Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiwa na watendaji wa afisi za mahakama, waendesha mashitaka na Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi, wakienda kwenye gereza  lililoko Kengeja wilaya ya Mkoani, ikiwa ni ziara maalumu
Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiwa na watendaji wa afisi za mahakama, waendesha mashitaka na Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi, wakiwa kwenye vikalio maalum, kwenye kambi ya askari magereza Kengeja wilaya ya Mkoani, kabla ya kuanza kuzungumza na wapiganaji na wanafunzi waliopo hapo
Kamanda Dhamana wa kambi ya wapiganaji wa askari wa magereza Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, Hafidh Haji Mcha, akiwakaribishwa watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar LZSC na ujumbe wao, wakati walipowatembelea kwenye kambi hiyo
Mwendesha Mashitaka kutoka afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Pemba, Seif Mohamed Khamis akifafanua jambo, mara baada ya wanafunzi wa gereza la Kengeja, kutaka maelezo ya ucheleweshaji wa hati za hukumu kwa ajili ya kukata rufaa
 Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Mohamed Hassan Ali, akieleza juhudi zilizochukuliwa na ZLSC katika kutoa elimu ya utawala bora, wakati timu ya watendaji hao walipokuwa kwenye gereza lilioko Kengeja wilaya ya Mkoani
Mratibu wa Kituo wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed akimkabidhi magazeti maalum Kamanda Mdhamini wa kambi ya askari chuo cha mafunzo Kengeja, wakati ujumbe wa ZLSC ulipofika kuwatembelea
Watendaji wa Kituo cha huduma za Sheria, wapigaji wa vyuo vya mafunzo Kengeje, hakimu, mwendesha mashitaka mtendaji wa Mamlaka ya kuzuia rushwa, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kazi.
 (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.