Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha AFP na Waziri Asiye Kuwa na Wizara Maalu Mhe. Said Soud Azungumza na Waandishi Kulani Kitendo cha Kungolewa Mikarafuu yake na Watu Wasio Julikana.

Mhe Said Soud Said Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP na Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya habari kisiwani Unguja, katika ukumbi wa Idara ya Habari Zanzibar, kulaani kitendo cha Baadhi ya Wananchi kisiwani Pemba kuingia katika shamba lake la mikarafuu kufanya hujuma ya kuingoa mikarafuu hiyo na minazi iliokuwa katika shamba lake katika kijiji cha cha Mgelema Wilaya ya Chake chake na kumsababishia hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kutokana na uharibifu huo uliofanywa na Watu hao. 
Mhe. Said Soud Said akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na waandishi kulani kitendo hicho cha uharibifu wa zao la taifa la karafuu. na kusema Serikali inalipigia kelele na kuliimarisha zao hilo la karafuu kuna baadhi ya wananchi wanaturudisha nyuma kwa kufanya uharibifu huu.
Waandishi wakiwa makini wakimsikiliza Mhe Said Soud Said wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.