Habari za Punde

Kikao cha Pamoja Kati ya Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Tanzania Mhe Dk Charles Tizeba Kuzungumzia Juu ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu.

Ofisi za Jengo la Mamlaka ya Bahari Kuu Fumba Zanzibar  
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Tanzania Bara Dk Charles Tizeba na Katibu Mkuu wake wakipitia taarifa ya Mamlaka ya Bahari Kuu kabla ya kuaza kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ya Tanzania Bara kilichofanyika katika Ukumbi za Ofisi za Mamlaka ya Bahari Kuu Fumba Zanzibar kuzugumzia changamoto zake.
Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe Hamad Rashid Mohammed akipitia taarifa ya Mamlaka ya Bahari Kuu kabla ya kuaza kwa kikao hicho cha pamoja kuzungumzia machangamoto zinazojitokea katika Mamlaka hiyo, aliyesimama Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bahari Kuu Tanzania Ndg Rashid B.Hoza. na mwenye kanzu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar akitoa maelezo kabla ya kuaza kwa mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo mbili, uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Mamlaka ya Bahari Kuu Fumba Zanzibar.
Maofisa wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Tanzania wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo wa pamoja katika Ukumbi wa Ofisi ya Mamlaka ya Bahari Kuu Fumba Zanzibar.

Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza wakati wa Mkutano huo wa pamoja akitowa taarifa ya changamoto inazozikabili Mamlaka hiyo ya Bahari Kuu Tanzania, akisisitiza jambo.kulia mwenye suti Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Tanzania Bara Mhe Dk Charles Tizeba, 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bahari Kuu Tanzania Ndg Rashid B Hoza akitowa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Bahari Kuu Tanzania wakati wa kikao hicho na changamoto wanazokutana nazo wakati wa kufuatilia meli zinazoingia Tanzania kuvua na utoaji wa leseni za uvuvi katika bahari Kuu ya Tanzania.
Mawaziri wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bahari Kuu Tanzania wakati wa mkutano huo wa pamoja kuimarisha ushirikiano katika ya pande hizi mbili kuimarisha na kudhibiti uvuvi katika bahari kuu ya Tanzania.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Tanzania Bara Mhe Dk Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo mbili za SMZ na SMT uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Mamlaka ya Bahari Kuu Fumba Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.