Habari za Punde

Maadhimisho ya Tamasha la Mzanzibari Fukuchani

Na Maryam Kidiko/Kijakazi Abdalla-Maelezo Zanzibar                            

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema lengo kuu la kufanywa tamasha la Utamaduni wa Mzanzibar ni kuwaunganisha wazanzibar katika kulinda na kudumisha utamaduni huo.

Hayo yameelezwa mshauri wa Raisi katika mambo ya utamaduni Chimbeni Kheri   katika ufungaji wa tamasha la 21la utamaduni wa mzanzibar huko Fukuchani Wilaya ya kaskazini  A”.                               

Amesema kuwa utamaduni huo pia unawakutanisha wazanzibar kutoka sehemu mabali mbali ili waweze kubadilishana mawazo juu ya njia bora ya kuendeleza utamaduni kupitia njia ya sanaa.

Aidha amesema utamaduni ni roho ya taifa hivyo unahitaji kuenziwa , kuendelezwa, kurithiwa na watoto wetu katika michezo mbali mbali ya kiutamaduni .

“ Utamaduni ni muhimu sana kwani hujenga afya ,kukuwa kwa kiakili na hupata ajira kwani dunia ya sasa inazingatia sekta ya sanaa na utamaduni katika ustawi wa maendeleo ya kimataifa.Alisema Chimbeni.

Hata hivyo ameeleza kuwa majanga mengi katika jamii hujitokeza kwa kuacha mila na desturi za kizanzibar hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuurejesha utamaduni wetu .

Sambamba na hayo amesema kuwa Serikali imeweka mazingira mzuri yakuwawezesha  Wasanii wa fani zote ili kuweza kunufaika na kazi zao ili kuweza kuchangia pato la taifa .

“Katika suala la utamaduni serikali imechukuwa hatua  madhubuti ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho sheria inayohusu mambo ya utamaduni ili iendane na mahitaji ya Jamii” Alisema mshauri huyo.

Nae Waziri waHabari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema Wizara yake itashirikaana na Wizara ya elimu kuhakikisha somo la utamaduni linarudi katika skuli ili watoto waweze kuzijuwa mila na utamaduni wao .

Waziri huyo amefafanuwa zaidi kuwa suala la utamaduni litaendelea kuwepo  na kuwa la kihistoria  na  kila mmoja anatakiwa kuwa balozi wa mwenziwe ili kuweza kuulinda utamaduni huo usipotee katika visiwa vyetu.


Sambamba na hayo Tamasha hilo limejumuisha michezo mbalimbali ya kiutamaduni ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Dumisha utamaduni na amani , piga vita udhalilishaji . 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.