Habari za Punde

Mgogoro wa Shamba la Wakfu Mgagadu, Mkoani Pemba

 AFISA Mdhamini wizara ya Nchi, Afisi Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba Massoud Ali Mohamed (nyuma), akiambatana na Mkuu wa kamisheni ya Wakfu na mali ya amana Pemba Ali Haji, wakiangalia mipaka ya shamba lenye mzozo liliopo Mgagadu wilaya ya Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mdhamini wizara ya Nchi, Afisi ya rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba Massoud Ali Mohamed akimfahamisha jambo, mmoja wa anaedai kuporwa shamba lake Khalid Mohamed Rashid wakati uongozi wa wizara hiyo pamoja na Kamisheni ya wakfu walipokuwa wakikagua shamba hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MOJA ya eneo la shamba lenye miti kadhaa ikiwa ni pamoja na mikarafuu, linalodaiwa kuibua mgogoro baina ya bwana Nassor Khalid na bwana Khalid Mohamed Rashid eneo la Mgagadu wilaya ya Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 UONGOZI wa wizara ya Nchi, afisi ya rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba, ukiongozwa na Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba Massoud Ali Mohamed asie na tai, wakati wakirudi kuangalia shamba la wakfu lililoibua mgogoro eneo la Magagdu wilaya ya Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mdhamini wizara ya Nchi, Afisi ya rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba Massoud Ali Mohamed wa Mgagadu wilaya ya Mkoani akifahamisha jambo bwana Nassor Khalid juu ya kukaa na familia yake, kumaliza mgogoro wa matumizi ya shamba la wakfu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.