Habari za Punde

Uzinduzi wa Tamasha la Jahazi la 19 Zanzibar Viwanja vya NgomeKongwe Zenj

MC Faruok akitowa maelezo wakati wa Uzindfuzi wa Tamasha la Jahazi la 19 lililozinduliwa jana usiku katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma. 
Wananchi wa Zanzibar na Wageni kutoka Nje ya Zanzibar wakiwasili katika ukumbi wa Uzinduzi wa Tamasha la Ziff. ndani ya Red Carpet
Wageni wakiingia katika viwanja vya Ngome Kongwe Zenj.
Mshiriki wa mafunzo ya kuandika script za michezo ya kuigiza Wankonja Kabunda kutoka Mkoani Rukwa Tanzania, ambaye anatumia ulimi kuandikia ni mmoja kati ya Vijana 15 waliofaulu kushiriki mafunzo hayo ya kuandaa script yanayotolewa na ZIFF katika Tamasha hili la 19. akiwasili katika viwanja vya Ngome Kongwe. wakati wa uzinduzin huo.
Mtunzi na Muigizaji wa Cinema za Kihindi kutoka India Kunal Kapool akiwasili katika viwanja vya Ngome Kongwe kuhudhuria uzinduzi huo.
Mambo ya Red Carpet hayo ndani ya Ziff Zenj. 
Watunzi wa film wakiwa katika Red Capet kutoka kushoto Rashid Lanie Kunal Kapool na Mandlakayise Dube kutoka Afrika ya Kusini. 
Mambo ya Red Carpet hayo kwa Wananchi waliofika katika uzinduzi wa Tamasha la 19 la ZIFF Zanzibar.
Vimwana wakijimwaga katika Red Carpet ndani ya Ngome Kongwe Zenj.


Miss Tourism 2015/2016, Willice Donald akiwa katika maonesho ya mavazi yalioandaliwa na Fashion &Desing Waiz Shelikindo wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la 19 la Nchi za Jahazi Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.
Desing Fashion Waiz Shelukindo akisalimia baada ya kumaliza kuonesha ubunifu wa mavazi alobuni wakati wa uzinduzi huo wa Tamasha la ZIFF jana usiku wakati wa uzinduzi wake. 
Msanii wa mchezo wa sarakasi kutoka Zanzibar kjana Maha akionesha ujasiri wake wakasti wa uzinduzi wa Tamasha la ZIFF Zanzibar. jana usiku.

CEO wa ZIFF Prof Martin Mhando akitowa maelezo wakati wa uzinduzi huo wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF na kutowa historia ya Tamasha hilo tangu kuaza kwa miaka 19 sasa linatimia   
Wananchi na Wageni mbalimbali kutoka Nje wakihudhulia Tamasha la Nchi za Jahazi katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha hilo na kutoa pongezo kwa Mashirika na Kampuni zilizojitokeza kudhamini Tamasha hilo la 19 na kuwatambulisha wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika jana usiku katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar jana 9-7-2016
Baadhi wa Wadhamini wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar wakitambulishwa wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe jana usiku.
CEO wa Kampuni ya Zanlink Mr. Sajay Raja akizungumza na kutowa shukrani kwa niaba ya wadhamini wa Tamasha hilo la 19 la ZIFF lililozinduliwa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.
Wasanii wa Ngoma ya Kilua wakionesha umahiri wa kucheza Ngoma hiyo wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Ziff jana.

Wananchi na Wageni kutoa Nje wakifuatilia Uzinduzi wa Tamasha hilo katika viwanja vya Ngome Kongwe jana usiku.
Mtunzi na Muigizaji wa Film kutoka Nchini India Mr Kunal Kapool akizungumza na kuwasalimia wananchi waliohudhuria Tamasha hilo wakati wa uzinduzi wake jana.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akielekea katika jukwaa kwa ajili ya uzinduzi wa Tamasha hilo jana usiku likiwa ni Tamasha la 19 tangu kuazishwa kwake hapo Zanzibar. 
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akihutubia wakati wa Uzindizi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar lililozinduliwa katika viwanja vya Ngomev Kongwe Zanzibar jana usiku na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali kutoka Nje ya Zanzibar.
Wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri wa Habari akihuubia wakati wa Uzinduzi huo. wa Tamasha la 19 la Nchi za Jahazi Zanzibar. 
Watunzi wa Film ya Kalushi kutoka Afrika Kusini wakitowa maelezo ya Film yao hiyo wakati uzinduzi wa film hiyo akizungumza ni Rashid Lanie na kushoto Mandlakarise Dube, wakiitambulisha film yao kabla ya kuaza kuoneshwa jana wakati wa uzinduzi wa Tamasha la ZIFF.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.