Habari za Punde

Muonekano wa Darajani Mpya Ujenzi wa Maduka ya Kisasa

Michoro ya ujenzi wa maduka ya Kisasa katika eneo la Darajani Makontena baada ya kuondolewa makontena hayo kwa kupisha ujenzi huu wa kileo kama inavyoonekana michoro ya eneo hilo la darajani litakavyokuwa baada ya ujenzi wake wa maduka ya kisasa.
Mhandishi Yassir Dicosta akitowa maelezo ya michoro ya ujenzi wa maduka ya kisasa katika eneo la darajani baada ya kuondolewa kwa makontena hayo, akitowa maelezo hayo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mhe Haji Omar Kheri alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo la darajani. 

2 comments:

  1. nimependa ni idea nzuri na ni kweli mji wetu lazima ubadilike, sio tukae na majengo ya zamani tu kisa nini mji wa kihistoria. idea hiyo nadhani inasaidia wageni Zaidi kuliko sisi wenyeji. Wacha tubadilishe mji wetu ili tufaidike sote wageni na wenyeji. Suali langu :: Jee tayari tumeshajipanga na fedha ipo ya kujenga hiyo darajani mpya??? Isijegeuka kule njia ya Fuoni tumefanya haraka ya kuvunja nyumba na kutanua barabara sasa hatma yake twala vumbi na ubovu wa barabara umezidi. Bora tungebaki na ule ule ulimi wa nyoka kuliko huu ulimi wa n'gombe uliopo sasa.
    Kama hakuna pesa bora tungewaachia wauza tende, chinga na makontena wakaendelea kupata riziki zako wakati tunasubiri fedha. Kama zipo Alhamdulillah twasubiri maendeleo.

    ReplyDelete
  2. hiyo ramani naona haifahamiki isije ikawa yale ya uwanja wa ndege tu, SMZ kutapeliwa inaonekana ni kitu rahisi sana

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.