Habari za Punde

ZLSC Pemba yafanya mafunzo ya siku mbili, kwa masheha na madiwani wa Wilaya ya Mkoani

 MRATIBU wa Mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akizungumza juu ya mafunzo hayo, kwa masheha na madiwani wa wilaya ya Mkoani, yaliofanyika mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MASHEHA na madiwani wa wilaya ya Mkoani, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdalla, hayupo pichani akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa masheha na madiwani hao juu ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).


MKUU wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa msheha na madiwani wa wilaya hiyo, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).   
 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada juu ya dhana ya wasaidizi wa sheria, mbele ya masheha na madiwani wa wilaya ya Mkoani, mafunzo hayo yalifanyika ZLSC mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

MWANASHERIA kutoka afisi ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Matar Zahoro akiwasilisha sheria ya tawala za mikoa kwa masheha na madiwani wa wilaya ya Mkoani, mafunzo yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba juu ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, (Picha na Haji Nassor, Pemba). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.