Habari za Punde

KLABU YA SIMBA YATOA FURSA KWA MAWAKALA MIKOANI KUUZA VIFAA VYA SIMBA.

Katika kupanua wigo wake wa kibiashara lakini pia katika kuwafikishia wanachama, wapenzi na mashabiki wake, Klabu ya Simba imeanzisha mpango maalumu wa kutafuta mawakala ambao watatambuliwa na klabu ya Simba ili kuweza kuuza bidhaa zake mbalimbali sehemu zote za Tanzania.

Katika kulifanikisha hilo Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula, ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara na masoko ya Klabu ya Simba ameelezea kwa undani dhima ya kuendesha zoezi hili la kutafuta mawakala kwa kusema ‘Klabu ya Simba ni moja kati ya klabu kubwa sana Barani Afrika na hii inaipa nguvu klabu hii si tu ndani ya Uwanja bali hata nje ya uwanja, sasa Klabu imeona ni vema kutawanya (Decentralized) upatikanaji wa huduma pamoja na vifaa vyote vyenye chapa ya Simba kwa kuanzia na kutafuta mawakala mbalimbali ambao wataingia mkataba na klabu ya Simba katika kulifanikisha hili, kama unavyojua hapa situ klabu itafaidika zaidi na chapa yake bali pia itakuwa imesaidia katika kuongeza ajira zaidi nchini kupitia mauzo ya bidhaa zenye chapa ya Simba. 
Hili ni zoezi endelevu na tumeanza kwa kutoa namba ambapo kama wewe ni mfanyabiashara na ungependa kuchangamkia fursa hii adhimu basi wakati ni huu na unaweza kupiga namba 0766 842 457 au kutumia barua pepe kupitia info@simbasports.co.tz na hapo unaweza kuongea nasi’.‘Uamuzi huu unalenga kusogeza upatikanaji wa jezi halisi za Simba kote Tanzania, kukuza ajira na pia kuiongezea Simba mapato. Maduka au wauzaji watangazwa kupitia mitandao ya Simba hivyo kutangaza zaidi biashara zao’

Sasa pia unaweza kununu jezi kupitia duka mtandao la Simba kupitia www.jumia.co.tz ambapo utanunua jezi popote ulipo na kwa gharama nafuu tutakuletea pale ulipo, alimalizia Imani Kajula Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa EAG Group.
Sasa ni muda wako ewe mfanyabiashara kutokea sehemu yoyote ulipo Tanzania kuchangamkia fursa hii adhimu ya kuwa wakala halali wa klabu ya Simba. Piga namba hii ili kuweza kupata maelekezo zaidi 0766 842 457. SIMBA NGUVU MOJA






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.