Wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba, wakiwa katika harakati za ukataji wa Tiketi za Azam Sealink,huko katika maeneo ya Chake Chake , kumekuwa na hofu ya usafiri kwa wakati huu hivyo wananchi wana hofu wakakosa usafiri kwa vile Chombo cha Usafiri wa majini kwa sasa ni kimoja baada ya kutokuwepo kwa MV Mapinduzi 2 .
Picha na Bakar Mussa -Pemba.
KUTOKUWEPO kwa meli ya Mv Mpinduzi II kwa zaidi ya
siku 10 sasa, kumepelekea usumbufu mkubwa kwa abira wanaohitaji usafiri wa
kwenda Unguja, kwa kutumia meli ya Mv Sealink pichani abiria wakiwa katika
foleni kusubiri kununua tiketi za meli ya Jumapili, huku zaidi ya abiria 150
wakiachwa na meli hiyo kwa kuwa na tiketi zisizofanana majina yao katika
vitambulisho vyao vya mzanzibari mkaazi.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
azam tena hizo tiketi zenu fanyeni watu wakate kwenyemtandao, sio kibiru tu mke wa mtu, mjane, mbakaji, barobaro wote hapo hapo, azzam kampuni kubwa
ReplyDelete