Na Salmin Juma - PEMBA
Ubovu wa miundo mbinu rafiki kwa ajili ya wawekezaji bado ni tatizo ambalo zinarudisha nyuma sekta ya uwekezaji kisiwani pemba .
Mkurugenzi mkaazi wa mamlaka ya uwekezaji zanzibar ( ZIPA) Fadhila Hassan Abdalla amesema mamlaka imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma hizo lakini bado hawajafanikiwa akutokana na ubovu wa miundo mbinu .
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akitoa taarifa kwa wajumbe wa kamati ya fedha , biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi walipofanya ziara ya kuyatembelea maeneo huru ya uwekezaji yaliyoko maziwangombe wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba .
Amesema kwamba kwa maeneo ya kiuchumi kisiwani pemba hayajaweza kufanya hivyo licha ya kwamba yametangazwa kwa muda mrefu .
Naye mwenyekiti wa kamati hiyo Yusssuf Hassan Idd ameishauri serikali kuimarisha huduma ya miundo mbinu katika maeneo huru yaliyotengwa kwa ajili ya uwezekezaji ili kusaidia pia kupatikana ajira kwa vijana.
0 Comments