Habari za Punde

Sheha aipa baraka Jumuia ya Maendeleo Chumbageni kuanza kazi


Na Haji Nassor, Pemba
UONGOZI wa shehia ya Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, umeupa baraka ya kuanza kazi Jumuia ya Maendeleo na Kupunguza Umaskini ya shehia hiyo, baada ya kujitanmbulisha kwake.
Akizungumza kwenye hafla ya kujitambulisha kwa uongozi huo, Sheha wa shehia hiyo Khamis Mohamed Nahoda, alisema yeye hana shaka na kuwataka viongozi wa Jumuia hiyo kufanya kazi zao kama walivyokusudia.
Alisema kila siku wamekuwa wakitakiwa na uongozi wa wilaya, kuwahamasishwa wananchi kujikusanya pamoja kwa lengo la kujikwamua na umaskinim, hivyo ameridhishwa na wazo la wanancho hao.
Sheha huyo alieleza kuwa, atakuwa bega kwa began a Jumuia na nyengine katika shehia yake, hasa kwa vile wanaisaidia serikali katika kupunguza wimbi la vinana wanaosubiri ajira serikali.
“Mimi nimehamasika na kuvutiwa mno, na wazo lenu la kujikukusanya pamoja kwa lengo la kujiletea maendeleo, sasa na mimi nitaitangaaza Jumuia hii kila kwenye vikao vyetu’’,alifafanua.
Hata hivyo amewataka viongozi hao, waache kufanya kazi kama nguvu ya soda, kwa kufa na kufufuka, maana wananchi na wanachama wenu wanaweza kuvunjika moyo.
Mapema Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Asha Mohamed Khamis, alimuomba sheha huyo kuwaangalia kwa jicho la huruma, ili wazo na ndoto zao zifanikiwe.
“Sisi tumekuja kujitambulisha kwako, lakini jitahidi sana pamoja na kazi zako, tuonyesha njia na pahala la kupita, ili ndoto na azma zetu zizae matunda’’,alifafanua.
Mapema Katibu wa Jumuia hiyo Saleh Abdalla Mohamed, alimpongeza sheha huyo kwa kuwapokea na kuwakubalia kuanza kazi kwa Jumuia hiyo, ndani ya shehia yake.
Nae Mwneyekiti wa Jumuia hiyo Khamis Juma Khamis, alisema ndio kwanza wanananza sasa, hivyo amemuomba sheha huyo asiche kuwakosoa, kuwashauri na kuwaelekeza ili wafikie dhamira zao.

Jumuia ya Maendeleo na Kupunguza Umaskini Shehia ya Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, ambayo inawanachama 35 hadi sasa, imeanzishwa mwezi Julai mwaka huu, kwa lengo la kujikwamua na umaskini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.