Habari za Punde

Timu ya Sumait Wajifua Ndani ya Uwanja wa Jomo Kenyatta.

Mashindano ya kumi ya michezo kwa Vyuo vikuu vya nchi za Afrika Mashariki yanatarajiwa kuanza rasmi kesho kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Jomo Kenyatta Juja Nairobi, nchini Kenya.Wakati mashindano hayo yakielekea kuanza kutimua vumbi lake asubuhi ya leo hii kikosi cha wachezaji wa chuo cha Sumait kutoka Chukwani Zanzibar kimeanza kujifua kwa ajili ya ngarambe hizo.


Wakiwa kwenye mazoezi hayo baadhi ya wasomi wa chuo cha Jomo Kenyatta sambamba na wakaazi wa eneo hilo walionekana kufurahishwa na Wazanzibari hao.


"Vijana wanaonekana wako sawa na wako na ari kubwa, nimefurahia vile wanafanya" alisema Ochieng Butui.

Kwa upande wake nahodha wa Sumait Mohamed Iddi Duchi alisema hali ya viwanja hairidhishi kutokana na kuwa kukumbwa na jua kali na kusababisha viwanja hivyo kuwa vikavu sana.

Kamati inayosimamia mashindano hayo huenda ikahamishia baadhi ya michezo hasa ya mpira wa miguu chuo jirani cha Kenyatta kutokana na kuthibitisha kuwepo kwa kasoro hizo.


Ratiba ya mashindano hayo inatarajiwa kutoka saa moja usiku wa leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.