Habari za Punde

Wananchi wahofia usalama wao kutokana na ubovu wa nyumba


Picha za Majumba ya Shirika la Nyumba za mtaa wa Polisi line Wete, zinazolalamikiwa kuwa ni mbovu na watu wanalipa kodi kama kawaida.

Picha na Zuhura Msabah -Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

WANANCHI wanaoishi mtaa wa Police line, shehia ya kipangani Wilaya ya Wete Pemba ambao  wamepangishwa katika nyumba za shirika la majumba ya Serekali Zanzibar, wamesema wanahofia usalama wao, kutokana na nyumba hizo kuwa ni mbovu, jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.
Walisema, nyumba hizo zilizojengwa tokea enzi za ukoloni hazijawahi kufanyiwa matengenezo makubwa ambapo mpaka sasa wakaazi wa nyumba hizo wako  katika mazingira hatarishi ya maisha yao.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakaazi wa nyumba hizo walisema, wamekuwa wakifanya matengenezo madogo madogo, ili kuweza kujikinga na athari zinazoweza kutokea ingawa haiwasaidii kutokana na nyumba hizo kuwa na ubovu wa kuopindukia.

“kipindi cha mvua huwa kama tuko chini ya muembe jinsi tunavyo vujiwa, hivyo tunakosa raha ya kulala kwani tunahofia kuangukiwa na viambaza vya nyumba”, walisema wakaazi hao.

Wakaazi hao waliliomba shirika hilo kuwaangalia kwa jicho la huruma kutokana na athari zinazoweza kutokea katika nyumba hizo.



Mmoja wa wakaazi hao ambae hakutaka kutajwa jina lake alisema awali ilivyokuwa idara ya Majenzi walikuwa wanatengeneza nyumba hizo na kuweza kukatizina katika kodi ingawa baada ya kuanzishwa shirika haikuwa hivyo.

“Ingelikuwa tunatengeneza kisha tunakatiziana kwenye kodi basi zisingekuwa mbovu kiasi kile maana ni hatari hasa kukiwa na upepona mvua.

Nae mkaazi mwengine (hakutaka jina lake litajwe) alisema kuwa, wamekuwa wakihofia usalama wao wakati kutokana na nyumba anayoishi kuanguka vigae, jambo ambalo linawatia hofu kuishi katika nyuma hizo.

“Kwa kweli ni mtihani mkubwa lakini hatuna la kufanya, Kwa nini hawatutengenezei hali kama hii, ukiwaita wanakwambia tunakuja na wakija basi ni muda wa kudai kodi, wanatuonesha nini tuseme”, alihoji mkaazi huyo.

Kwa upande wa mkaazi alieishi kwa zaidi ya miaka 36 aliema kuwa tayari amefanya matengenezo makubwa katika nyumba hiyo kwa gharama zake mwenyewe huku akilipa kodi kama kawaida, jambo ambalo ninamkwaza sana.

“Huku nilipe kodi, huku nifanye matengezezo makubwa, nimejenga nguzo za choo, nimetia bati, mlango na nimetia saruji nyumba nzima,  hali yenyewe ni ya kimasikini, naomba mutuhurumie”, alisema.

Mkaazi mwengine alisema kuwa, pamoja na ubovu wa nyumba wanazoishi wamekuwa wakilipia gharama sawa na nyumba za horofa za maendeleo (ftate), jambo ambalo hazilingani kutokana na ubovu wa nyumba wanazoishi wao.

“Awali tulikuwa tunalipa 22,500 tokea kuundwa shirika tunalipia  45,000 kila mwezi kwahivyo tunaiomba serekali itupunguzie au ituuzie” alisema.

Akizungumia athari zinazotokezea katika nyumba hizo alisema ni pamoja na vyoo kubomokeza maji na kuja juu, kuanguka kwa vigae vilivyoezekewa, kuanguka kwa masinbodi na hatibae kupelekea kutokea kwa shoti ya umeme wakati wa mvua.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Majumba Pemba  Suleiman Hamad Omar alisema nymbaza maeneo mengi zipo katka hali mbaya ambapo nyengine hazikaliki ingawa watu wanakaakutokana kuwa hawana namna nengine yakutafuta maazi yakuishi.

“Nyumba za Polis Lain kwa kweli asilimia 70 ni mbovu na zinahitaji kuvunjwa nakujengwaupya na shirika limeelekeza kujenga nyumba za kileo na za gorofa, kwa sasa Shirika linafanya tathmini kwa nyumba zote”, Alisema Mratib huyo.

Alisema kuwa walishawahi kupata malalamiko kwa wakaazi wa polisi lain Wete, lakini shirika haliwezi kutowa mamilioni kadhaa kwakufanyamatengenezo nyumba mbovu ambayo inahitaji kuvunjwa na kujengwa  upya.

Aidha alisema kuwa nyumba za polis lain haziuzwi na kuwahakikishia wakaazi hao kwamba hawatoondoshwa pindi nyumba hizo zitakapojengwa upya.

“Shirika bado ni changalakini tumejipanga kufanya matengenezo madogo madogo ya muda lakini malengo yetu ni kujenga upya nyumba za kimaendeleo”, alieleza.

Wakaazi wa Police line Wete wanakabiliwa na tatizo la ubovu wa nyumba wanazoishi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.