Na Mwandishi wetu.

Hii ni kutokana na tukio la usiku wa kuamkia leo la kukatwa migomba isiyopungua 38 mali ya Bi shufaa Asaa Mwombwa kwa kile kinachodaiwa kua ni itikadi za kisiasa.
Akikagua shamba la migomba hiyo huko Nyali Mtambwe mara baada ya kupata taarifa hizo Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wapili wa Rais , Mohamed Aboud ameonyesha kukerwa na tukio hilo huku akisema kua serikali itahakikisha inawatia mbaroni wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo na sheria zitachukuliwa dhidi yao ili kukomesha hali hiyo.
Amesema kama ni uchaguzi umeshamalizika na Dk shein ndie raisi wa Zanzibar, hivyo vitendo vya kukata miti na kuhujumu haviwezi kumuondoa madarakani.
Kwengineko Uwondwe Mtambwe nako miche ya miti mbalimbali isiyopungua 1100 ya wananchi wa kaya maskini zinazodhaminiwa na TASAF imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na watu wasio fahamika.

Alipoulizwa na waziri huyo juu ya wanaodhaniwa kua watendaji wa tukio hilo amesema kua watu hao wanawajua hasa kwakua hawataki kuona mashirikino na mafanikio katika shuhuli hizo.
Waziri Aboud kwa upande wake amewasisitiza wananchi hao kuendelea na kazi zao hizo za kimaendeleo huku akiwa akisema kua serikali watashirikiana na mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania na kamishna wa jeshi hilo Zanzibar kuleta timu kutoka makao makuu Dar es salaam ije ifanye kazi ya kuchunguza nani wahusika wa tukio hilo na wote watakao tambuliwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua nyengine waziri huyo amesema kua watafanya kura ya siri kwa wananchi wa maeneo hayo ili kueleza nani wahusika wa tukio hilo ili wapate kubainika na sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment