Habari za Punde

Tambua athari za Pampers kwa watotoTumezoea kuona kila nyumba yenye mtoto kuwa na pempasi kama ndio nguo ya ndani ambazo hutumika kuvishwa watoto kwaajli ya kuzuia kinyesi na mikojo kutapakaa.

Katika ulimwengu wa sasa wazazi wamekuwa watumiaji wakubwa pemasi kama kurahisisha matumizi ya mipira, nepi na matambara kuwavisha.

Mnamo mwaka wa 2000 pempasi ziliingia na kushamiriTanzania bara na visiwa Zanzibar nakupelekea kila Mzazi mwenye mtoto kutamani kununua kwajili ya kumvisha mwanawe ili pale anapomaliza kuitumia kuitupa kama njia rahisi inayomuepusha na kazi ya kufua.

Awali tulikuwa tunawaona wazazi walilazimika kuwa na kazi kubwa ya kufua nepi na matambara mara kwa mara baada ya kutumia, hali hii ilikuwa ni salama kwani walikuwa wakiwakagua mara kwa mara japo ilikuwa ni usumbufu kwani walikuwa wakitumia mda mkubwa kwa ajili ya kusafisha nepi hizo.

Wakati huu wapempasi tunaona maisha kubadilika sana sijui kutokana na kujitia shughuli au kupenda kurahisisha mambo maana unamuona mzazi anamvisha pempasi mtoto usiku na analala nayo mpaka asubuhi hana hata muda wa kumkagua na kumbadilishawa. Kwavile yeye anaona hasiki harufu tu basi huoni hakuna tatizo, kumbe kwake hakuna tatizo ila kwa mtoto anamjengea matatizo makubwa ya kiafya.

Tunawashuhudia watoto wetu wengi wa sasa wamekuwa wanaathirika zaidi na pempasi na kupata Maradhi mbali mbali kama Uchovu na kudumaa afya zao kutokana na maradhi yatokanayo kwa kuwavisha pempasi kwa muda mrefu bila kuwabadilisha.

Wazazi wengi hawana elimu juu ya matumizi ya pempasi ambapo wanaamini baada ya kumvisha mtoto ndio basi tena mpaka muda wakumaliza shughuli zako ndipo atamkagua mtoto.

Kukosekana kwa elimu kunaweza kupelekea athari mbali mbali indapo utamvisha mtoto kwa muda mrefu bila ya kumbadisha kama vile madaktari wanavyosema Pempasi zina madhara makubwa kwa watoto na yanaweza kupelekea madhara Magonjwa kama U.T.I (Urinary Tract Imfections), Derminatitis, Ugomba, fangasi na Uwasho sehemu za siri.

Mabadiliko ya PH (Kiwango cha tindikali) hasa katika sehemu ya haja kubwa kutokana na unyevu nyevu unaokaa kwa muda mrefu na hata kupelekea kifo endapo mtoto hajawahiwa kufanyiwa matibabu.

Kutokana na ushambuliaji wa vidudu vinavyotoka kwenye kinyesi hupelekea Mtoto kushambuliwa mfumo mzima wa uzazi na kufanya ashindwe kuwa na kizazi (Tasa).
Hili ni tatizo kubwa sana litakalopelekea kuwa na taifa la baadae lenye Watu wengi wavivu na wasiyo na Uzazi (Tasa).

Najua Taifa letu kwasasa linaanza kulisimamisha Taifa la kuwajibika "Hapa Kazi" lakini kama hatutowatunza watoto wetu kwa maradhi yatokanayo na pempasi ambayo yanayoweza kuepukika tutapata Taifa la baadae vivu na lenye kusizia ovyo ofisini.

Uwasho unaweza kumfanya mtoto kukosa furaha na kumpelekea kulia mara kwa mara. Pia hali hiyo humfanya mtoto kuzohofisha afya yake na ukuwaji, kukomaa kwa Mtoto, Uchovu, maumivu ya mgongo, kuharibika kwa viungo vya uzazi (kupelekea utasa), kushindwa kufanya kazi kwa figo, fangasi ambazo husabisha muwasho mara kwa mara, kuchubuka kwa ngozi kwenye sehemu za siri za mtoto na hupelekea kuingia kwa fangasi tumboni.

Mbali na magonjwa mbalimbali yanayowapata watoto hata hivyo pempasi bado zimekuwa chanzo cha uchafunzi wa mazingira ambapo wazazi wamekuwa wakizitupa ovyo katika maeneo bila ya kuzihifadhi.

Wataalamu wa Afya Duniani wanasema kuwa pempasi ni chanzo chengine cha maradhi ya mripuko (Kipindupindu) ambapo kuna baadhi ya wazizi na walezi wengine huzitupa pempasi kwenye Vyanzo vya maji na kusababisha kusambaa vinyesi katika maji na baadae kupelekea maradhi ya kipindupindu, matumbo na kuharisha Damu.

Najua kwa madhingira tuliyojizowesha ni ngumu kubadilika kwa rahisi ila tukiamua tunaweza kwani hatuna budi wazazi na walezi kufuata ushauri wa madaktari kwa matumizi sahihi na kuchukua tahadhari ya kuwavisha watoto pempasi kwa muda mrefu na kuwakagua mara kwa mara ili kuepusha kupata madhara yatokanayo na pempasi kutokana na kuwavisha kwa muda mrefu.

Pia kwa upande wa mazingira nawasihi wazazi mara baada ya kutumia pempasi zao wanatakiwa kuzihifadhi sehemu maalumu ambazo hazitokuwa zikileta uchafuzi wa madhingira na athari kwa binadaamu au kupelekea kuzagaa mitani ovyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.