Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Taifa ya Jangombe na Kilimani City Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amani Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe Imeshinda kwa BAO 4 - 1.

Benchi la Ufundi la Timu ya Kilimani Cty wakiwa na majonzi baada ya Timu yao kukubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Jangombe katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Katika mchezo huo timu zote zimeonesha mchezo mzuri na kushambuliana kwa zamu itabidi wachezaji wa Timu ya Kilimani City wajilaumu kwa washambuliaji wao kukosa mabao mengi wakiwa golini kwa wapinzani wao timu ya Jangombo. 

 Katika dakika ya 22 ya mchezo huo kipindi cha kwanza timu ya Taifa ya Jangombe ikiongoza kwa bao moja 

 Katika kipindi cha pili cha mchezo huo mchezaji wake Mesa Apinga aliipatia bao timu yake katika dakika ya 49 ya mchezo huo Katika kipindi hicho cha pili Timu ya Taifa ya Jangombe imeandika bao lake la tatu kipitia mshambuliaji wake Ali Badru katika dakika ya 51 ya mchezo huo.

Timu ya Kilimani City walirekebisha makosa yao katika dakika ya 66 ya mchezo huo kipindi cha pili waliweza kupata bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Abubakari Ahmeid kuunganisha smpira ya krosi. Timu ya Taifa ya Jangombe imefunga karamu yake ya mabao kupitia kwa mchezaji wake Ali Badru katika dakika ya 81 ya mchezo huo na hadi mwisho timu ya Taifa ya Jangombe imetoka na ushindi wa bao 4-1



Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Jangombe Saleh Mussa Maisara akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.









No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.