Habari za Punde

Mradi wa Tasaf Awamu ya Tatu Kujenga Msingi wa Kupitishia Maji katika Mabonde ya Mpunga Mwera Kuwasaidia Walengwa wa Kaya Maskini Zanzibar

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Mihayo Juma Nhunga akizungumza na Walengwa wa Kaya Maskini katika Shehia ya Mwera, wakati wa uchimbaji wa msingi wa maji katika Mradi wa Tasaf 3 katika mabonde ya mpunga mwera kusaidia kilimo hicho kwa Wananchi welengwa wa mradi huo kujiongezea kipato kupitia Mradi huo.
Wananchi wa Shehia ya Mwera walengwa wa Kaya Masikini wakimsikiliza Naibu Waziri Mhe Mihayo Nhunga akizungumza na wananchi hao baada ya kazi ya uchimbaji wa mchingi wa kupitishia maji katika mashamba ya mabonde ya mpunga mwera yakiwa chini ya Mradi huo kuwasaidia Wananchi wa Kaya Masikini Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Mwera akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uchimbaji wa msingi wa maji katika mabonde ya mpunga mwera.

Mkurugenzi Idara ya Shughuli za Serikali ya SMZ na SMT na Uratibu Zanzibar Ndg Khalid Bakari Hamrani akizungumza na Wananchi hao wakati wa hafla hiyo ya uchimbaji wa msingi wa maji kumwagilia mashamba ya mpunga katika bonde la mwera Zanzibar. Mradi huo ukiwa chini ya Mradi wa Tasaf 3 kusaidia Kaya Masikini Zanzibar. 





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.