Habari za Punde

Fundo karibuni kupata Umeme Zeco yafunga Transfoma

 MAFUNDI wa shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakifunga Tansfoma katika kijiji cha Ndooni Kisiwani Fundo, ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha kisiwa hicho kinapata huduma ya Umeme ya uhakika.



(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAFUNDI wa Shrika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakipachika Tansfoma katika moja ya vituo huko katika kijii cha Kimeleani Kisiwani Fundo Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Na Mwandishi wetu

Zoezi la usambazaji wa nguvu ya umeme katika Kisiwa cha FUNDO linaendelea kwa kasi huku uongozi wa shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ukiahidi kulikamisha kwa wakati.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia maendeleo ya zoezi hilo afisa uhusiano wa ZECO Pemba Amour Salim Massoud amesema tayari wameshafunga trasfoma nne na kujenga line kubwa na kwasasa wanalenga kujenga line ndogo kwa ajili ya kuwashushia wananchi.

Amesema mafundi wa shirika kwa kushikiana na wananchi wa Fundo wamekuwa wakifanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha zoezi hilo linamalizika kwa muda uliopangwa.

Nao baadhi ya wananchi wa fundo wameelezea kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na kuwaomba mafundi wa shirika la umeme ZECO kujitahidi kukamilisha uwekaji wa line hizo ili waanze kukamilisha usajili na kujiungia huduma hiyo ya umeme.


Aidha wameuomba uongozi wa ZECO kutoa elimu kwa wananchi wa FUNDO juu ya matumizi salama ya umeme na kuepuka ajali zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.