Habari za Punde

Mohammed Ali wa kipindi maarufu cha jicho pevu nchini Kenya kujiunga na siasa


Mwandishi Mahiri wa Habari za Uchunguzi nchini Kenya, Mohammed Ali anayefahamika kwa Makala za Jicho Pevu ametangaza kujiuzulu kutoka taaluma ya kufichua maovu ya kiutawala na jamii na kujiunga na siasa.


Mohammed katika mtandao wake wa Twitter ameandika "Kwa miaka 10 mfululizo nimekuwa nikisimama nanyi kuzidisha sauti zenu za kuangaishwa. 

Sasa ni wakati wangu wa kuwauliza, msimame nami katika harakati zangu za kuwania ubunge wa Nyali kwa tiketi ya ODM". 

Ameahidi kuwa akitimiza ndoto hiyo atakuwa mshirikishi mkuu wa utawala wa haki kwa Wakenya wote bila ubaguzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.