Habari za Punde

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Maghari Unguja Kamishna Msaidi wa Polisi Zanzibar Hassan Nasir, akizungumza na waandishi wa habari Ofisini Kwake Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Maghari muembe madena Unguja kuhusiana na tukio la kifo cha Mwananchi Mohammed Abdallah Haji mkaazi wa meli mnne Zanzibar aliyejaribu kumuokoa mpanda pikipiki aliyezama katika eneo la kibonde mzungu baada kuteleza na kuingia katika bonde hilo Kijana Paulo Salum akijaribu kumuokoa. 
Marehemu alikuwa akipita njia na gari yake na kushuka kutowa msaada huo na mauti kumkutwa kwa kuza katika eneo hilo na maiti yake kuokolewa na Kikosi cha KMKM Zanzibar. 
   Aliyekwenda kumuokoa Kijana aliyekuwa akipita katika barabara hiyo wakati akipishana na gari hatimae aliteleza na kutumbyukia katika bonde hilo linalopita katika barabara hiyo Kijana Paulo Salum alikimbizwa hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kupata matibabu na naendelea vizuri baada ya matibabu yake.
Wiki mbili zilizopita ilitokea ajali ya kuzama mpanda vespa marehemu Abass Anass Haji.
Jeshi la Polisi limepiga marufuku kupita vyombo vya moto vya maringi mawili katika marabara hiyo iliopita katika bonde hilo la kibindemzungu.
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo ikitolewa na Kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Kamanda Hassan Nasir. 
Kamando wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi akisikiliza maswali ya waandishi wa habari Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.