Habari za Punde

Nafasi za kazi ya Ualimu

NAFASI ZA KAZI KWA SKULI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Skuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Walimu wa Skuli za Maandalizi:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘A’ 15
KASKAZINI ‘B’ 6
MAGHARIBI ‘A’ 4
MAGHARIBI ‘B’ 5
KATI 9
KUSINI 5
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 7
CHAKE CHAKE 4
WETE 4
MICHEWENI 11

Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu fani ya Ualimu wa Maandalizi katika ngazi ya Cheti kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Walimu wa Skuli za Msingi:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘A’ 2
KASKAZINI ‘B’ 2
MAGHARIBI ‘A’ 3
MAGHARIBI ‘B’ 3
KATI 3
KUSINI 2
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 5
CHAKE CHAKE 1
WETE 2
MICHEWENI 4


Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Diploma ya Msingi (Diploma in Primary Education) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3. Walimu wa Skuli za Sekondari:

WILAYA ZA UNGUJA
WILAYA NAFASI
KASKAZINI ‘B’ 2
KUSINI 2
WILAYA ZA PEMBA
MKOANI 3
CHAKE CHAKE 2
WETE 2
MICHEWENI 3

Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amesomea Shahada ya Ualimu katika masomo ya Histroy, English na Kiswahili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Mwalimu wa Sayansi Chake Chake Pemba “Nafasi 4”
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amesomea Diploma ya Ualimu wa Sayansi au awe amefaulu vizuri elimu ya Kidato cha Sita katika masomo ya Chemistry, Biology au Physics

5. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Habari na Mawasiliano (ICT) Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano’ (ICT) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Jinsi ya Kuomba:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo ya Ualimu. 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Muombaji anaombwa kuiainisha Wilaya anayoiomba 
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.