Habari za Punde

Taifa ya Jango'mbe Ndembendembe yakutana na kipigo cha pili mfululizo

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa  Jang’ombe imekubali kichapo cha pili mfululizo jioni ya leo kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora baada ya kufungwa na JKU bao 1-0 kwenye uwanja wa Amaan.

Bao pekee la JKU lililopeleka kilio kwa Taifa limefungwa na Mbarouk Chande katika dakika ya 82.

Huo ni mchezo wa pili mfululizo kupoteza kwa Taifa kufuatia mchezo wa awali kufungwa na Jang’ombe boys mabao 3-0.

Mbali ya kutoshinda Taifa lakini pia hawajafunga hata bao moja katika dakika 180 walizocheza kwenye michezo miwili ya mwanzo.

Mchezo mwengine jioni ya leo umepigwa huko Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani ambapo Jamhuri imekamata usukani baada ya kuwa na alama 6 kufuatia ushindi wa leo walipoichapa Okapi mabao 3-0.

MZUNGUKO WA TATU UTAENDELEA JUMAPILI NA JUMATATU

Jumapili 21/5/2017 Jang’ombe Boys v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 21/5/2017 Mwenge v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumatatu 22/5/2017 Zimamoto v/s Taifa Jang’ombe, saa 10:00 Amaan.
Jumatatu 22/5/2017 Jamhuri v/s Kizimbani, saa 10:00 Gombani.

Baada ya hapo ligi hiyo itasimama na kupisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo itakuja kuendelea Mzunguko wa nne mpaka imalizike Mwezi huo wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.