Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Masauni Ashirikisha Wadau wa Maendeleo Kueneza Huduma ya Maji Kikwajuni.

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini,  Alvaro Rodriges (kushoto), alipotembelea Mradi wa Maji Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein miaka miwili iliyopita ikiwa ni juhudi za Mbunge huyo kushirikisha wadau katika kuhudumia na kutatua kero mbali mbali za wananchi wa jimbo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi  Mohamed  Elyas. na anayefuata ni Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman
Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman akimuonyesha Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodrigues (wa kwanza kushoto),ramani ya mpango wa uboreshaji huduma ya maji katika jimbo la Kikwajuni. Mratibu huyo amefika jimboni hapo ikiwa ni juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad  Masauni (wa tatu kushoto)katika juhudi zake za kutatua changa moto za huduma ya maji kwa wananchi
Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas, akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Kikwajuni kwa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodrigues alipotembelea mradi huo uliopo katika jimbo la Kikwajuni,Zanzibar
MratibuwaUmojawaMataifa(UN)nchini,  Alvaro Rodrigues, akiangaliamojayamabombayanayotumikakusafirishamajikwendakwenyemaeneombalimbalijimboniKikwajuniikiwanisehemuyaushirikianonaMbungewaJimbohilo,Mhandisi Hamad Masauni() katikakuhakikishaanamalizatatizo la upungufuwamajijimbonihapo

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas (kulia) wakati wakiondoka baada ya kumuongoza Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na wadau katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni. PichanaAbubakariAkida

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.