Na.Haji Nassor. Pemba.
MTOTO Mussa Khamis Abdalla (14)
mkaazi wa Michezani wilaya ya Mkoani Pemba, amekuwa mtu wa kwanza kufanyia upasuaji
mdogo na matibabu ya kuvinjika mguu bure, kupitia vifaa vya kisasa kutoka
China, vilivyopo hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani.
Mtoto huyo
alifikishwa hospitalini hapo, akiwa amevunjika mfupa wa mguu wa kushoto, baada
ya kupata ajali akiwa kwenye shughuli zake za kawaida, na kupokelewa kisha
kuanza kuandaliwa taratibu za matibabu kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Vifaa hivyo
ambavyo kwa Afrika Mashariki vipo kwenye hospitali hiyo pekee, kama sio kuwepo
familia ya mtoto huyo ingelazimika kuvifuata India na kutumia zaidi ya shilingi
milioni 15.
Daktari mkuu
kutoka China wa kitengo cha Mifupa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Abdalla Mzee
Mkoani, dk Yang Xiao, alisema matibabu hayo yamechukua muda wa dakika 55 hadi
kumalizika.
Alisema mfupa
huo wa mguu wa kushoto, umepasuka na kama sio kuwepo kwa vifaa hivyo vya kisasa,
engelazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuondoa nyama za mguu, na kisha mfupa
na kuanza kuutibu.
Dk Yang,
alieleza kuwa utabibu huo wa zamani kwa sasa haupo tena kwenye hospitali hiyo,
hasa baada ya serikali ya watu wa China, kukabidhi vifaa hivyo vya kisasa mwezi
uliopita, mbapo kwa Afrika Mashariki, vipo hospitalini hapo pekee.
“Vifaa hivi
vya kisasa ndio vya kwanza kwa Afrika Mashariki, na hapa matibabu yake ni bure,
lakini India vipo na matibabu pamoja na usafiri wa mtu mmoja ni shilingi
milioni 15”,alifafanua.
Hata hivyo
alisema operesheni hiyo ambayo aliongoza yeye, alikuwa karibu sana na madaktari
wazalendo, ambapo lengo la baadae ni kuhakikisha wanaweza kuvitumia mara
watakapoondoka.
Aliongeza
kuwa, mashine hiyo hata ikikaa zaidi ya mwaka kama haijapata mtu alievunjika,
haiathiriki ingawa alisema uzoefu unaonyesha kila ifikapo msimu wa uvunaji wa
zao la karafuu, waathirika huwa wengi.
Akizungumza
na mwandishi w ahabari hizi motto huyo, alisema anashangaa kuona siku moja
kabla baada ya matibabu anaweza kuunyanyua mguu wake.
“Leo (jana)
niko adhali sana sina yale maumivu makali niliokuja nayo, maana kama nilietiwa
mguu mpya, sihisi hasa kama nna athari ya ndani”,alisema.
Baba mzazi wa
motto huyo Khamis Abdalla Haji, aliwapongeza madaktari hao kwa ujemedari wao
mkubwa wa kuokoa mguu wa mtoto, ambapo hakutarajia kwamba ungezekena.
“Mimi nilijua mwanangu ameshapa ulemavu wa maisha, na wakati natoka nyumbani nilijua ni safari ya Muhimbili jinsi mguu ulivyokuwa, lakini nashukuru”,alisema.
“Mimi nilijua mwanangu ameshapa ulemavu wa maisha, na wakati natoka nyumbani nilijua ni safari ya Muhimbili jinsi mguu ulivyokuwa, lakini nashukuru”,alisema.
Daktari
Makame Chirau anaefanyakazi kwenye kitengo cha mifupa hospitalini hapo, alisema
matumizi ya vifaa hivyo vya kisasa, ni mazuri na yataepusha wanaovujika kwa
kiaisi kikubwa kuwekewa piop ipo au vyuma.
“Zamani
ilikuwa kila anaekuja amevunjika anawekewa vyuma ndani ya mwili au pio pio,
lakini sasa baada ya kupata vifaa hivi, hali imekuwa ya kisasa
zaidi”,alifafanua.
Mmoja kati
ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari hizi, Haji Makame Hilali wa
Mkoani, alisema hiyo ni hatua moja wapo kubwa ya kuimarisha huduma za afya
kwenye hospitali hiyo ya Mkoa.
Nae Ashura
Hija Yussuf, alisema hata baada ya kuondoka kwa madaktari hao kutoka China,
vifaa hivyo ni vyema vikaendelea kutumika na kuondoa suala la fedha kidogo
kabla ya huduma.
Vifaa hivyo
vya kisasa ambavyo vinathamani ya shilingi milioni 60, vilitolewa mwezi
uliopita na hospitali ya Wuxi no 2 ya watu wa China, ambapo vifaa hivyo kwa
Afrika Mashiriki pekee, vipo hospitalini hapo.
Tunapswa kumshukuru Allah kwa hatua hiyo. Ingawa bado najiuliza ikiwa vifaa hivyo vya kisasa kabisa gharama zake ni 60milioni, hivi kwa miaka yooooote hiyo Serikali yetu imeshindwa kabisa kupata fedha hizo ili kuwasaidia wanyonge sisi kupata huduma bora? Na hata kwa hospital nyengine za Zanzibar bado kama tuna nia njema khasa ya kuwasaidia wanyonge wa nchi hii million kama hizo tunao uwezo wa kuzipsta, la msingi kuwsjali wananchi
ReplyDelete