Habari za Punde

Uzinduzi wa Ripoti za Haki za Binadamu Zanzibar ya Mwaka 2016.

MWENYEKITI wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Msibe Ali Bakari akizungdua kitabu cha Ripoti ya Haki za Binadamu Zanzibar ya mwaka 2016, iliozinduliwa katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. 
MGENI Rasmin katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu Zanzibar Mhe. Jaji Msibe Ali Bakari akionesha  kitabu cha Ripoti hiyo baada ya kukizindua katika ukumbi wa Kituo hicho akiwa na Viongozi wa meza kuu.


MKURUGENZI wa Mashtaka Zanzibar Mhe Ibrahim Mzee akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binaadamu Zanzibar kwa mwaka 2016, akiongoza  mjadala huo uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar .
 BAADHI ya Washiriki wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu Zanzibar wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria kijangwani Zanzibar.
AFISA Mipango wa ZLSC  akiwasilisha Ripoti ya Haki za Binadamu kwa wajumbe wa mkutano huo baada ya kuzinduliwa rasmin na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Msibe Ali Bakari, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Zanzibar
WASHIRIKI wa Mkutano wa Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu Zanzibar ya mwaka 2016 wakisoma ripoti hiyo baada ya uzinduzi wake uliofanyika katika kituo hicho kijangwani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.