Habari za Punde

CAF yampongeza Machupa kwa kuendesha kozi ya makocha wa Magolikipa

Kocha wa Makipa Saleh Ahmed Seif "machupa"

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” limefurahishwa kwa kitendo cha Mkufunzi wao wa Makocha wa Magolikipa Saleh Ahmed Seif “Machupa” kuharakisha kuendesha kozi ya msingi ya Makocha wa Magolikipa Visiwani Zanzibar na kusema huo ni uzalendo wa hali ya juu kabisa.

Hayo yamesemwa na Makamo wa Urais wa ZFA Unguja, Mzee Zam Ali wakati anazungumza na Mtandao huu siku chache baada ya kumalizika kwa kozi hiyo ambayo ilianza Jumatano ya July 5, 2017 na kumalizika Jumanne ya July 11, 2017 katika ukumbi wa uwanja wa Amaan Mjini Unguja ambapo makocha 29 walihitimu kozi hiyo.

Zam amesema CAF wamefurahishwa mno kusikia Machupa kaendesha kozi ambapo wamesema katika Wakufunzi wao wote waliyohitimu kozi ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa nchini Cameroon basi Machupa yeye ndio mzalendo namba moja kuliko wenzake.

“CAF waliposikia Machupa anaendesha kozi wametutumia ujumbe katika barua pepe yetu ZFA kwa kumpongeza na kusema kuwa huo ni uzalendo wa hali ya juu kwa kitendo hicho cha Machupa kwani katika kozi yao waliyosoma kule Cameroon yeye ndie wa mwanzo kuendesha kozi mapema nchini kwao”. Alisema Zam.

Machupa ni Mkufunzi pekee nchini Tanzania aliyehitimu Kozi ya CAF ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa wa ndani kozi ambayo aliisomea nchini Cameroon mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu, Machupa pia ameshahitimu kozi ya FIFA ya Ukocha wa Magolikipa ya hatua ya juu (Advanced Level) na pia ana Leseni “B” ya Ukocha inayotambuliwa na CAF.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.