Habari za Punde

Kamati ya soka la Ufukweni Zanzibar kuandaa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika MasharikiNa: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Kamati ya soka la ufukweni visiwani Zanzibar imevialika vilabu vitatu kutoka Uganda kwaajili ya kucheza Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki ya Beach Soka Mashindano ambayo yanatarajia kuanza rasmi 4/9/2017 katika Fukwe za Bububu Bambuu Visiwani hapa.

Akizungumza na Mtandao huu Rais wa Beach Soka Visiwani Zanzibar Ali Sharifu “Adolf” amesema kwa vile Afrika Mashariki nzima nchi zenye ligi kuu ya Beach soka ni wao Zanzibar na Uganda tu ambapo nchini nyengine hawana ligi hiyo ndio mana wakavialika vilabu vya Uganda vitatu na vya Zanzibar vitatu kisha watacheza Mashindano hayo.

“Unajua kwa Afrika Mashariki nzima Zanzibar na Uganda pekeyetu ndo tunaocheza ligi kuu ya Beach soka, nchi nyengine hawana ligi kuu labda mabonanza tu na timu zao za Taifa, lakini nchi mbili hizi ndo zinazocheza ndo mana tumevialika vilabu vya Uganda kucheza na Zanzibar kwaajili ya kumtafuta Bingwa wa Beach Soka Afrika Mashariki nzima”. Alisema Adolf.


 Timu 6 zitakazoshiriki katika Mashindano hayo ni Malindi, Green River na Lavister kutoka Zanzibar na kutoka Uganda ni Makerere University, Mutesa 1 Royal University na St. Laurence University.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.