Habari za Punde

Ligi Kuu Zanzibar kuanza kesho mzunguko wa 6


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mzunguko wa 6 wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora utaanza rasmi kesho Jumatatu ya July 17, 2017 kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Mwenge watacheza na Zimamoto katika uwanja wa Gombani saa10:00 za jioni.

Kesho kutwa Jumanne ya July 18, 2017 mechi nyengine 3 ambapo Okapi watasukumana na Taifa ya Jang’ombe katika uwanja wa Gombani saa 10:00 za jioni, na katika uwanja wa Amaan JKU watakipiga na Kizimbani saa 10:00 za jioni, kisha saa 1:00 za usiku Jang'ombe boys dhidi ya Jamhuri.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya 8 bora ni kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.