Habari za Punde

Mchezaji wa Mafunzo Arejea Uwanjani Baada ya Kupona Majeraha ya Kuchomwa Kisu na Kukosa Kucheza Mwaka Mzima.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mlinzi wa Kati wa timu ya Soka ya Mafunzo Kheri Salum Kheri “Chivu” amerejea mazoezi katika kikosi chake na kuanza kujifua na wenzake baada ya kukosa Mwaka mzima.

Beki huyo amerudi uwanjani baada ya kukaa nje msimu mzima uliopita wa mwaka 2016-2017 ambapo alipata tatizo kufuatia kuchomwa kisu na kijana mmoja anatuhumiwa kuwa ni muhalifu huko nyumbani kwao Migombani Mjini Unguja ambapo tukio hilo lilitokea karibu ya mwaka sasa, na awali alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja kisha kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Kairuki na Muhimbili huko Tanzania bara.

“Narudi uwanjani katika kipindi muhimu ambacho timu inanihitaji kutokana na ugumu wa ligi 2, kama unavyojua sasa kuna ligi 1 na 2 na sisi Mafunzo tupo ligi 2 hivyo nataka kupigana tuipeleke Mafunzo ligi 1, wenzangu wamenimis sana mwaka mzima lakini kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu nimepoa na mazoezi nimeshaanza na wenzangu”.  Alisema Kheri.

Kheri ni kaka wa damu wa Abdallah Salum Kheri (Sebo) Beki wa Azam FC na Omar Salum Kheri “Inzaghi” mlinzi wa kushoto wa African Lyon ndugu zake wote wakicheza soka Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.