Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (wapili kulia) akionyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis
Massawe (kulia), jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani humo ambalo limekwama
ujenzi wake, lililopo mjini Babati mkoani humo. Masauni amemaliza ziara yake ya
siku mbili mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu
Kamishna, Juliette Sagamiko (kushoto) alipokua anatoa maelezo kuhusu Jengo la
Makao Makuu ya Uhamiaji mkoani humo (linaloonekana nyuma ya viongozi hao),
ambalo lipo katika hatua ya mwisho kukamilika lakini limekwama kuendelea na
ujenzi wake. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Francis Massawe.
Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kushoto), akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara. Watatu kulia ni Kamanda wa Jeshi hilo,
mkoani humo, Heriel Kimaro.Masauni amemaliza ziara yake
ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya
Wizara yake
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,
Francis Massawe, wakati alipokua akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Jeshi hilo,ofisini
kwake mkoani humo. Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humokwa
kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
No comments:
Post a Comment