Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Atembelea Viwanda Jijini Tanga leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro alipowasili kukizindua maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiakata utepe kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mwijage wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mwandishi wa habari wa TBC Bi. Vumilia Mwasha baada ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakicheza ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakikata utepe kwenye sherehe za  uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga  ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.