Habari za Punde

Table Tennis yapata uongozi mpya , Kisandu ndani



Na: Abubakar Khatib, Zanzibar.

Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar “Zanzibar Table Tennis Association (ZTTA)” kimepata viongozi wapya watakaongoza kipindi cha miaka minne ijayo baada ya kufanyika Uchaguzi katika Ukumbi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.

Katibu wa Kamati ya Uchaguzi Suleiman Haji (Kibabu)amewatangaza washindi kwa nafasi saba zilizogambaniwa katika Uchaguzi huo ambapo kwa nafasi zote wagombea walikuwa mmoja mmoja na wapiga kura walikuwa 16 hivyo kura zilipigwa kwa ndio na hapana.

Kibabu amemtangaza Latifa Daud Jussa kuwa Mwenyekiti mpya kwenye chama hicho baada ya kura 14 kumkubali na 2 kumkataa, nafasi ya Makamo Mwenyekiti akashinda Faki Ali Faki baada ya kura zote 16 kumkubali, nafasi ya katibu amejitokeza Ahmed Abdallah kashinda kwa kura 16 zote kumkubali, huku katibu msaidizi ameshinda Omar Mohd Othman baada ya kura 16 zote kumkubali.

Wakati huo huo Mwanamama Asha Haji Ame ameshinda nafasi ya mhasibu mkuu baada ya kupata kura 16 zote kumkubali, Abubakar Khatib Haji (Kisandu) nae ameshinda nafasi ya Mhasibu Msaidizi baada ya kura 14 kumkubali na kura 2 zilimkataa huku Salum Ramadhan Abdallah akishinda nafasi ya mjumbe baada ya kura zote 16 kumkubali.

Viongozi hao wataongoza kwa muda wa miaka 4 ijayo ndipo utafanyika uchaguzi mwengine kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.