Habari za Punde

Walimu wa maskuli wapatiwa mafunzo ya siku tano ya Ufundi na Hisabati

 Mratibu wa Jumuiya ya kumuendeleza mtoto wa kike kielimu (FAWE) Hinda Abdalla Ajmy  akizungumza na walimu na wanafunzi  walioshiriki mafunzo ya siku tano ya Ufundi na Hisabati katika Hoteli ya Africa House Shangani, Mjini Zanzibar.
 Mhandisi wa ujenzi  Talha Masoud akiwaonesha washiriki wa mafunzo hayo michoro ya majengo aliyobuni na kuwataka wanafunzi wa kike kujitokeza kujiunga na fani hiyo kwani inasoko kubwa hivi sasa. 
 Mtaalamu wa  Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (ICT) Raya Said Khalifa akiwasisitiza wanafunzi wa kike kujiunga na fani hiyo ili kwenda na wakati wa sasa wa sayansi na teknolojia.
 Wanafunzi wa skuli ya wanawake Tumekuja wakifanya majaribio ya huduma ya kwanza katika mafunzo ya siku tano ya sayansi yaliyofanyika Hoteli ya Africa House Shangani Zanzibar.
 Walimu wa skuli  walioshiriki  mafunzo hayo wakifuatilia majaribio ya kisayansi yaliyokuwa yakifanywa na washiriki wenzao.

Mgeni rasmi Afuwa Mohammed akiyafunga mafunzo ya siku tano kuhusu masomo ya sayansi yatokanayo na engineering na hisabati mara tuu baada ya kuwahutubia.

(PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.