Habari za Punde

Miembeni City yaendelea kuchapwa Ligi Kuu Zenj, JKU kama kawaida ushindi tu


Na: Abubakar Khatib, Unguja.

Mzunguko wa Pili wa Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja umeanza leo katika uwanja wa Amaan kwa kupigwa michezo miwili.

Saa 8 za mchana mabingwa watetezi JKU wakaichapa Chuoni mabao 3-2 ambapo mabao ya JKU yamefungwa na Shomari Waziri dakika ya 12, Ali Haji Said (Zege) dakika 48 na Nassor Matar dakika ya 64, wakati mabao ya Chuoni yamefungwa na Charles Chinonso dakika ya 24 na Hamad Mshamata dakika ya 29.

Saa 10 za jioni Miembeni City ikaendelea kuchapwa katika ligi hiyo baada ya leo kupigwa na Mafunzo bao 1-0.

Bao pekee la Mafunzo limefungwa na Ali Othman dakika ya 27.ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumatatu 16/10/2017 saa 8:00 za mchana Taifa ya Jang’ombe vs Polisi na  saa 10:00 za jioni KVZ vs Zimamoto

Jumanne 17/10/2017 saa 8:00 za mchana Kipanga vs Charawe

Jumanne 17/10/2017 saa 10:00 za jioni KMKM vs Kilimani City

Jumatano 18/10/2017 saa 10:00 za jioni Black Sailors vs Jang’ombe Boys

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.