Habari za Punde

SIMBA WAANZA RASMI KUWATAFUTIA DAWA YANGA BAADA YA KUWASILI ZANZIBAR, WAPIGA TIZI JESHINI

Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi mepesi jioni ya leo katika uwanja wa Jeshini Migombani Mjini Unguja ambapo wapo Kisiwani hapa kwaajili ya Kambi maalum kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka ya Tanzania bara dhidi ya Watani wao Yanga utakaopigwa Oktoba 28, 2017 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salam.

Jumla ya wachezaji 24 wa Simba pamoja na viongozi 
wao wamewasili Unguja asubuhi ya leo wakitokea ijini Dar es salam kwa furaha baada ya Jumamosi iliyopita kuwachapa 4-0 Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba wataendelea kufanya mazoezi kila siku asubuhi kuanzia saa 3:00 katika uwanja wa Amaan na saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Jeshini Migombani.
Kikosi hicho kinachonolewa na Mkameroon Joseph Omog pamoja na msaidizi wake mpya Mburundi Masoud Djuma Irambona kimefikia kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.