Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Kimalazimishwa Sare na Timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini Unguja Katika Mchezo Wake wa Kujipima Nguvu Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kilicholazimishwa sare na Timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini Unguja katika mchezo wake wa kwanza majaribio uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar ikijiandaa na michuano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwezi Ujao. Timu ya 
Taifa ya Zanzibar imepanga katika Kundi linaloshirikisha Timu za Kenya, Tanzania Bara, Rwanda na Libya.
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar katikati Mohammed Issa akijiandaa kumiliki mpira huku mabeki wa Timu ya Wilaya ya Mjini Suweid Juma kushoto na Ali Humud kulia wakijiandaa kumzuiya, wakati wa mchezio wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Mwalimu Mohammed akijiandaa kumiliki mpira huku beki wa Timu ya Wilaya ya Mjini Ali Juma akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika Uwabnja wa Amani Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
KIPA wa Timu ya Wilaya ya Mjini Juma Haji akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakati wa mchezo wao Timu ya Taifa kujipima nguvu kujiandaa na michuano ya chalenji Nchini Kenya mwezi ujao
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Wilaya ya Mjini Hassan Ali akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Hereos wakati wa mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu kujiandaa na michuano ya Chalenji Nchini Kenya mwezi ujao, mchezo huo umefanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kilicholazimishwa sare na Timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini Unguja katika mchezo wake wa kwanza majaribio uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar ikijiandaa na michuano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwezi Ujao. Timu ya
Taifa ya Zanzibar imepanga katika Kundi linaloshirikisha Timu za Kenya, Tanzania Bara, Rwanda na Libya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.