Habari za Punde

Kocha Salahi aanza kazi na Malkia wa Zanzibar


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

KIKOSI kamili cha Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Wanawake (Zanzibar Queens) kimeanza mazoezi rasmi kikiwa chini ya bosi mpya wa ufundi, Mohammed Ali Salahi (Richkard), mazoezi ambayo yalianza saa 12:30 za asubuhi katika uwanja wa Amaan. 

Zanzibar Queens inajiandaa kwenda nchini Rwanda kwenye Mashindano ya CECAFA Woman Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu ambapo kikosi hicho kimepania msimu huu kufanya vyema tofauti na mwaka jana ambapo Zanzibar ndio timu ya kwanza kuaga rasmi mashindano baada ya kufungwa michezo yote mitatu na kufikisha idadi kubwa ya mabao ya kufungwa 30-1 kwenye michezo yote hiyo.

Wachezaji 20 wanaonda kikosi hicho msimu huu ni :-

WALINDA MLANGO
Salma Abdallah (Green Queens)
Hajra Abdallah (Jumbi)
Mtumwa (New Generation Queens)

WALINZI 
Hawa Ali (New Generation Queens)
Mtumwa Khatib (Women Fighter)
Aziza Mwadini (New Generation Queens)
Flora Kayanda (Jumbi)
Safaa Makirikiri (New Generation Queens)
Neema Suleiman (Jumbi)

VIUNGO
Mwajuma Ali (Jumbi)
Nasrin Mohd (Women Fighter)
Riziki Abdallah "Chadole" (Jumbi)
Aziza Ali (Jumbi)
Sijali Abdallah (Green Queens)

WASHAMBULIAJI 
Mwajuma Abdallah (New Generation Queens)
Shadida Abdallah (Women Fighter)
Neema Machano (Jumbi)
Dawa Haji (Women Fighter)
Sabah Hashim "Mess" (New Generation Queens)
Greece Ronald (Green Queens)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.