Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) akikabidhi
vifaa vya kufanyia usafi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi
Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya
usafi katika eneo la hospitali hiyo iliyopo Zanzibar hivi karibuni. Zantel
ilikabidhi vifaa vyenye jumala ya thamani ya Sh.400, 000 hospitalini hapo.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha akizungumza na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani (Mwenye
fulana ya bluu) wakati wa zoezi la kufanya usafi na kukabidhi vifaa hospitalini
hapo hivi karibuni mjini Zanzibar. Mkurugenzi huyo ambaye aliambatana na baadhi
ya wafanyakazi wa Zantel alikabidhi vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, ndoo na
mafyekeo vyenye jumla ya thamani ya Sh. 400,000/= kwa ajili ya kuimarisha mfumo
wa usafi na kuzuia maambukizi kwa watu wanaofika hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja
Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani (Mwenye fulana ya bluu kushoto) akitoa neno la
Shukrani kwa Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) na
wafanyakazi wote wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kufanya usafi na
kukabidhi vifaa vya usafi vyenye jumala ya thamani ya Sh.400,000 hospitalini
hapo hivi karibuni mjini Zanzibar.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel
wakishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, zoezi
ambalo lilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. Tofauti na kufanya usafi,
Zantel ilikabidhi vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, ndoo na mafyekeo vyenye jumla
ya thamani ya Sh. 400,000/= kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa usafi na kuzuia
maambukizi kwa watu wanaofika hospitalini hapo.

No comments:
Post a Comment