Habari za Punde

Wananchi Visiwani Zanzibar Wakishiriki na Kuungana na Wanafamilia Katika Mazishi ya Wapiganaji Wetu.

Leo ilikuwa ni siku ya huzuni kwa Watanzania hususan kwa Wazanzibari ambapo wapiganaji (JWTZ) wetu kutoka Zanzibar 9 tuliwaaga. Mmoja kati ya hao waliofariki huko DRC anaitwa Koplo Issa Mussa ambae alizikwa katika kijiji cha Ndijani, Wilaya ya Kati huko Mkoa wa Kusini Unguja. Katika maziko hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwakilishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. Mupumzike kwa Amani Mashujaa wetu #Tanzania #Zanzibar
 Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said na Waziri wa Afya Zanzibar wakishiriki katika mazishi ya mmoja wa Wanajeshi aliyefariki katika mapambano na waasi Nchini Congo wakilinda Amaani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.