Habari za Punde

Waziri Kiongozi mstaafu aweka jiwe la msingi kituo cha Afya cha Jeshi katika Kambi ya JKU Msaani Waziri Kiongozi Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha, akifunguwa Pazia kuashiri uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya ya JKU Msaani Pemba, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

 Waziri Kiongozi Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha, akibadilishana mawazo na Dk, Machano Issa Mohammed , huko katika hfla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Kituo cha Afya Msaani Pemba, ikiwa ni miongoni mwa Shamra za
miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.


 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar , Kanal, Ali Mtumweni Khamis, akieleza machache juu ya kazi kuu ya Jeshi hilo mbele ya Waziri Kiongozi Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha , huko katika Kambi ya JKU Msaani Pemba, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe na Msingi la Kituo cha Afya cha Jeshi hilo , ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Katibu mkuu Tawala za Mikao na Idara maalum za SMZ, Radhia Rashid , akitowa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa Kituo hicho cha Afya cha JKU Msaani Pemba , wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Kituo hicho
ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Naibu Waziri Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalumu zaSMZ, Shamata Shaame Khamis, akitowa maelezo machache katika mnasaba wa shuhuli hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha , kuweka Jiwe la msingi Kituo cha afya cha JKU Msaani , ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi .

 Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,akiwahutubia wananchi na Wapiganaji wa JKU na Viongozi mbali waliohudhuria katika sherehe ya uwekaji wa Jiwe la msingi la kituo cha Afya cha Jeshi hilo huko katika Kambi ya JKU Msaani , ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Shamsi Vuai Nahodha, akipanda mti huko katika Kambi ya JKU Msaani Pemba, mara baada ya kuweka Jiwe la msingi kituo cha Afya Kambini hapo , ikiwa ni
miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.


PICHA NA SAID ABRAHAMAN- PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.