Habari za Punde

BI Hekima avamiwa na Wezi nyumbani kwake atoa malalamiko yake

Na Bi Hekima

Asubuhi ya majuzi nimeamka na kukuta hali inayoashiria tukio la wizi uliofanyika kupitia uani wa nyumba yangu. 

Kuna sehemu ya massage ubavuni mwa ua inaelekea wamevunjiwa. 

Pia kuna ishara kuwa aliyeiba pia alipanda juu kwangu maana ngazi nimezikuta chafu zinaalama za miguu yenye tope. 

Suala la Wala unga na wezi kuingia  watakavyo nimelisemea sana kwa mamlaka zote husika miaka zaidi ya 7 sasa na mpaka leo hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa kwa sababu kadhia yangu inawahusu watoto wa 'wanamapinduzi' na kwa kauli zao niende popote haiwi lolote! 

Usalama wangu na wa Mali yangu uko mashakani. 

Nishaibiwa sana tu na ukienda kwenye vyombo husika wahusika wanalindwa. Hakuna heshma wala haki labda kauli za majukwaani tu. 

Uwazi uliopo Kwenye nyumba zote mbili ni wa kutengenezwa ili kuruhusu wahalifu kufanya uhalifu. 

Ukizingatia suala zima la usalama na faragha ya mwenye Nyumba  hakuna sababu ya msingi kuruhusu nyumba hizo za jirani ziwe na uwazi wa kuingia na kutoka uani kwangu.

Kukaidi kuchukua hatua kurekebisha hali hii ili kunihakikishia usalama unatafsirika kuwa mamlaka zinaridhia uvunjifu wote unaotokea. 

Na ieleweke hivyo maana kila jambo au anasingiziwa Baniani mbaya au watu wasiojulikana wakati watu Tunajitahidi kukosoa na kutoa taarifa. Mamlaka zinachagua nani kumsikiliza na kuchukua hatua muafaka kunusuru janga kabla halijatokea!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.