Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein Aufungua Ukumbi Mpya wa SUZA Leo.

Jengo Jipya la Ukumbi wa Chuo KikuuTaifa Zanzibar SUZA ambalo limefunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA , ukumbi huo umefanyika mahafali ya kwanza kufanyika katika ukumbi huo baada ya kufunguliwa rasmin leo na kutumika kwa hafla ya Mahafali ya 13  yamefanyika katika Ukumbi huo leo.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hassan Khatib alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha SUZA kuhudhuria mahafali ya 13 ya Chuoi hicho na kuufungua Ukumbi Mpya.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Rai,alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha SUZA kuhudhuria mahafali ya 13 ya Chuoi hicho na kuufungua Ukumbi Mpya.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha SUZA kuhudhuria mahafali ya 13 ya Chuoi Iddi, hicho na kuufungua Ukumbi Mpya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Ukumbi wa Mikutano la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA uliopewa jina la Dk. Ali Mohamed Shein Hall Tunguu Zanzibar, kulia Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Rai na kushoto Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wake. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuuzindua Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Zanzibar.kushoto Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ni Wairi wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) Profesa Idris Rai, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakimsikiliza Dk. Shein, baada ya kuuzindua ukumbi huo mpya wa SUZA Tunguu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.