NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
KINYANGANYIRO cha kuwania nafasi nne za juu katika ligi
kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba, bado imezidi kuwa ngumu kwa vilabu ambazo vipo
katika nafasi hiyo, kufuatia wavuvi wa kojani Timu ya Shaba kufanikiwa kuuzima
mwenge kwa bado 3-1.
Mchezo
uliopigwa katika uwanja wa michezo Gombani Huku ukishuhudiwa na mashabiki wengi
wa soka, kutokana na timu hizo kujenga uhasama kila zinapokutana.
Shaba
imeshuka uwanjani ikiwa na kisasi na mwenge kwa madai imeifanyia fitina hadi
kutolewa katika mashindano ya kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Mchezo
huo uliochezeshwa na mwamuzi Hassan Abdalla Geri, huku ukionekana kutaka
kumshinda katika dakika za mwisho, kufuatia wachezaji wa timu hizo kuanza
kutembezeana buti na kushindwa kuwaonya kwa kadi za manjano.
Kipindi
cha kwanza kilianz akwa kasi kubwa huku kila timu imkihitaji ushindi, ambapo
shaba imeshuka kiwanjani ikiw ana alama 29 ikishika nafasi ya tano, Mwenge
ikiwa na alama 35 ikishika nafasi ya pili.
Shaba
waliweza kupata bao la kwanza kupitia kwa Omar Shamte dakika ya 21, bao
lililodumu kwa dakika nne tu kufuatia mchezaji Yussuf Said kuisawazishia Mwenge
dakika 24.
Kuingia
kwa goli hilo pia liliweza kudumua kwa dakika nne tu, kufuatia mchezaji Salim
Juma Ali, alipoweza kuwanyanyua mashabiki wa shaba na kuanza kurindima uwanjani
hapo, baada ya kuipatia shaba bao la pili dakika 28.
Kuingia
kwa magoli hayo mwenge na shaba ziliweza kucheza kwa umakini mkubwa, kwa kila
timu kutokuruhusu goli jengine mlangoni mwake, huku kuyafanya magoli hayo
kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi
cha pili kilirudi kwa kasi kubwa, huku mwenge wakiutawala sana mchezo katika
kipindi hicho, kwa kutaka kusawazisha goli, lakini ngome za walinzi wa timu
hizo kuwa imara.
Hata
hivyo mabadiliko ya wachezaji wa timu hizo, yaliweza kuisaidia shaba dakika ya
81 walipopata penant ambapo mchezaji Salim Juma Ali alipobeba jukumu hilo, kwa
kufanikiwa kuipatia shaba goli la tatu na mchezaji huyo kutimiza magoli 9
aliyofunga hadi sasa.
Kwa
matokeo hayo shaba imefikisha alama 32, mwenge ikibakiwa na alama 35, ligi hiyo
itaendelea tena leo (kesho) kwa timu ya Opec kuwakabili chipkizi katika uwanja
wa Gombani.
No comments:
Post a Comment