Habari za Punde

Wanaohama nyumba za kiwanda cha sukari watakiwa kuacha kuzifanyia hujuma


Na Abdullah Mfaume, wilaya ya kasakazini b                                                                                                
Mkuu wa wilaya ya Kaskazini B bw.Rajab Ali Rajab amewataka wananchi wanaohama katika nyumba za kiwanda cha sukari Mahonda kuwacha kuzifanyia hujuma nyumba hizo ili ziwe katika hali ya usalama.

Wito huo ameutowa huko Mahonda Kizota wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wanaondelea kuka a katika nyumba hizo.

Amesema ana taarifa za kina za kuwa nyumba zilizohamwa zinafanyiwa hujuma kama vile kutolewa nyaya za umeme,madirisha na kung’olewa milango kwa hivyo kila aliyefanya hivyo atakapobainika hatuwa za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Rajab amesema si jambo la busara na ni kinyume na nidhamu za makaazi kufanya vitendo hivyo hata kama wanaofanya hivyo walifanya matengenezo lakini ni wazi gharama za matengenezo waliyofanya hayalingani na thamani ya muda walioishi katika nyumba hizo.

Nae katibu tawala wa wilaya ya Kaskazini B Makame Machano haji amewataka wananchi wanaoendelea kukaa katika nyumba hizo za starling wajiandae na  kuhama kwani nyumba zote zinatakiwa zirejeshwe serikalini.

Amesema anafahamu kuwa  ni jambo gumu wananchi kuhama katika nyumba hizo kwa kuwa tayari wameshazowea kukaa lakini hakuna budi kufuata agizo kama serikali inavyoelekeza.

Amewafahamisha wananchi hao  kuwa kuamriwa kuhama katika nyumba hizo si jambo la uonevu au kuchikiwa na serekali bali sheria na utaratibu ndivyo  vinavyoelekeza.

Ameongeza kuwa serekali ya wilaya ya kaskazini b itaendelea kuwahuduma wananchi hao kama kawaida bila ya kuwabaguwa kwani seriskali haina chuki na mtu na itaendelea kuwapenda wananchi wake.

Sheha wa shehia ya Mahonda, Alhaj Bakari Juma amesema pamoja na vitendo vya uhalifu vinavyo fanywa pia kumekuwa kukifanywa uharibifu wa mazingira kama vile kukatwa miti na uchimbaji wa mchanga katika maeneo ya nyumba hizo.

Nao wananchi waliohama na wanaoendelea kukaa wamekiri kuwepo kwa uharibifu huo na kuitaka serikali isimamie utaratibu ikiwemo  muda wa kuhama waliobakia na kuwapa taarifa mapema itakapofika wakati wa kuondoka na  kuzingatia matumizi ya taasisi za maendeleo na za kidini kama vile msikiti,skuli,madrasa na visima.

Jumla ya kaya 41 zilizotakiwa kuhama katika awamu  ya kwanza tayari zimeshatekeleza agizo hilo na kwa sasa kaya 118 zimebakia na kuendelea kuishi bila ya kujuwa khatma yao itakuwa lini lakini wameshapewa tahadhari siku yoyote wakitakiwa kuhama na wao watekeleze  agizo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.