Bakar Mussa, Pemba
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, inayoongozwa na Rais wa Dkt, Ali Mohammed Shein,
inaongozwa bila ya ubaguzi wa aina
yoyote na kwa kufuata misingi ya Katiba ya Zanzibar na inaendelea kuwaletea
maendeleo Wananchi wake kwa kufuata ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015-2020.
Akizungumza
na Uongozi wa Serikali , Kamati ya Ulinzi na Usalama na masheha wa Mkoa wa
Kusini Pemba Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Said Soud Said, huko katika Ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake,
alisema wale Viongozi wa Vyama vya Siasa wanaotumia majukwaa ya kisiasa na kuwadanganya Wananchi kuwa Serikali ya
Dkt, Shein, inaongozwa kwa misingi ya ubaguzi
ni sawa na kekebehi juhudi
zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar za
kuwaletea maendeleo Wananchi .
Alieleza
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , inayoongozwa na Dkt, Shein, chini ya chama
Mapinduzi imekuwa ikitekeleza ahadi ilizozitowa katika Ilani ya Uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015-2020 ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Unguja na Pemba katika
Sekta zote muhimu za Kijamii bila ya kuangalia itikadi zao walizonazo.
Soud,
aliwataka Masheha na Wananchi kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono na
kumuamini Dkt, Ali Mohammed Shein, juu
ya Uongozi wake wenye hekima na busara zinazomuwezesha kuongoza Zanzibar kwa
misingi ya Demokrasia.
“
Wale Viongozi wa Vyama vya Siasa wanaopita na kusema nchi hii , haina maendeleo
kwa vile inaongozwa kwa misingi ya ubaguzi niwatu wasiokuwa na dira ya
maendeleo na nikutafuta mtaji wa kisiasa kwani hakuna Mwananchi asieona
maendeleo hayo kwa nyanja tafauti tafauti ,” alieleza.
Alifahamisha
kuwa maendeleo yalioko Pemba katika kipindi cha utawala wa Dkt, Ali Mohamed
Shein, ni ya kupigiwa mfano ambayo hayana ubaguzi , na hajawahi kuwepo hata
katika awamu zilizopita na haya yamekuja baada ya kuwepo Amani na utulivu ndani
ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Kwa
upande wake , Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanziba, Juma Ali Khatib, aliwaonya Viongozi wa Vyama vya Siasa kwa kutoyatumia
majukwa ya kisiasa kwa kujijengea umaarufu huku wakiwa hadaa Wananchi Kisiwani
Pemba , kwamba kutakuwa na mbadala wa Dkt, Shein na atatangwaza Kiongozi wa
Upinzani.
Alisema
hakuna mbadala wa Dkt, Ali Mohammed Shein, mpaka Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Alifahamisha
kuwa wale Viongozi wa vyama vya Kisiasa wanaokaa wakiwahubiria Wananchi Siasa
na kuwaacha wakitekeleza majukumu yao ya kujitafutia maendeleo kwani wakati wa
kuhubiri mambo hayo ni mwaka 2020 na sio wakati huu.
“
Wananchi musikubali kugaiwa kwa misingi ya itikadi za Kisiasa bali , iungeni
mkono Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , inayoongozwa na Dkt, Ali Mohammed Shein,
kwani Serikali imetumia fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi yasiokuwa
na shubha ya ubaguzi wowote,” alieleza.
Juma
, alisema kuna baadhi ya Viongozi wamekuwa wakipita Kisiwani Pemba , na
kuwadanganya Wananchi kuwa ajira
zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zinatolewa kwa ubaguzi hayo ni
upotoshaji kwani ajira za Serikali zinatolewa kwa uwazi na kutangazwa katika
vyombo vya habari na kila mwenye sifa huomba na kupatiwa ajira kwa mujibu wa
sifa zinazotakiwa na taasisi husika.
Hivyo
aliwasihi Viongozi wa Vyama vya siasa kujaribu kuongoza Vyama vyao kwa kuiga hekma
na busara za Dkt, Ali Mohammed Shein, na sio kutumia majukwaa ya kisiasa kwa
kuwagawa Wananchi na kuichukia Serikali yao.
No comments:
Post a Comment