Habari za Punde

Tangazo la Ajira Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za mitaa na Idara Maalum SMZ

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ


Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika Idara na Mikoa mbali mbali Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

IDARA YA URATIBU TAWALA ZA MIKOA - UNGUJA:

1.Afisa Serikali za Mitaa Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala wa Serikali za Mitaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI - UNGUJA:

2.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari

OFISI YA MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA:

3.Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.

5.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunza ya ulinzi kutoka JKU au JKT.

6.Mtunza Ghala Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji Ghala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

OFISI YA MKUU WA WILAYA YA KATI UNGUJA:

7.Tarishi Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari

8.Dereva Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na awe amepata Leseni ya Udereva.
•Awe amepata mafunzo ya Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.

OFISI YA MKUU WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA:

10.Afisa Biashara Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Biashara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

BARAZA LA MJI MKOANI PEMBA:

11.Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

12.Wasafishaji Mji Daraja la III “Nafasi 3”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
Jinsi ya Kuomba:

•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. 

Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. 

Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.

g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 27 Aprili, 2018 wakati wa saa za kazi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.