WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akifungua Jengo Jipya la kuhifadhia Dawa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar ambalo limejengwa kwa msaada wa Mfuko wa dunia Global Fund Support .
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akifungua Jengo Jipya la kuhifadhia Dawa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar ambalo limejengwa kwa msaada wa Mfuko wa dunia Global Fund Support .
MUONEKANO wa Jengo Jipya la kuhifadhia Dawa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja liliopo karibu na Mapinduzi Kongwe.
MABOXI ya Dawa yakiwa yamehifadhiwa kwenye Jengo jipya la kuhifadhia Dawa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa Zaharan Ali Hamad akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa Jengo hilo.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akionesha aina ya Dawa alizozikamata maduka ya nje, Dawa ambazo haziruhusiwi kuuzwa.(Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar.)
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amezindua Jengo la kuhifadhia Dawa katika Hospital ya rufaa ya Mnazimmoja ambalo litatumika katika kuimarisha huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya Shilingi Millioni 600 ambazo ni msaada kutoka katika Mfuko wa dunia Global Fund Support.
Akizungumza na watendaji wa Wizara walioshiriki uzinduzi huo Waziri Hamad amesema jengo hilo litasaidia sana kupunguza malalamiko ya upungufu wa Dawa yanayotolewa na wananchi katika Hosptali hiyo.
Amewataka watendaji kuhakikisha wanaweka mifumo imara itakayoonesha aina ya Dawa zilizopo na zinazokaribia kumaliza ili Serikali ichukue jukumu lake la kuzileta Dawa hizo.
Hata hivyo Waziri Hamad ameendelea kuwakumbusha watendaji hao kuwa, hatochoka kufanya ziara mbalimbali za kukagua utendaji wa Wafanyakazi hasa Madaktari na Wauguzi.
Amesema amedhamiria kuhakikisha Wananchi wanapata matibabu yanayofaa bila aina yoyote ya manyanyaso ikiwemo lugha chafu kutoka kwa wahudumu.
Aidha ameendelea kuonya wale wote wanaondelea kuuza Dawa za Serikali kinyume na sheria wajiandae kukumbana na mkono wa sheria.
“Hili la wanaouza Dawa za Serikali mitaani na wale wanaotoa lugha chafu kwa Wananchi wanaoenda kutafuta matibabu sitokuwa na muhali nalo, lazima tuwanyooshe” alionya Waziri Hamad
Awali akitoa maelezo ya ujenzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Zaharan Ali Hamad akielezea chimbuko la ujenzi huo alisema waliomba msaada kutoka Global Fund kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya dawa katika Hospital hiyo.
Amesema eneo lililokuwa likitumika kuhifadhiwa Dawa kwa wakati huo halikutosheleza na kupelekea upungufu wa adawa kwa baadhi ya wakati kutokana na kukosekana kwa eneo la kuzihifadhia dawa hizo.
Hivyo Mkurugenzi Zaharan aliongeza kuwa kujengwa kwa jengo hilo kutawapunguzia Wafamasia kuchukua Dawa zinazotosheleza kwa kipindi kirefu kutoka katika Bohari ya Dawa na kuzihifadhi kwa pamoja katika Hospital hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mnazimmoja Dkt. Ali Salim Ali aliahidi kutoa mashirikiano ikiwemo kulitunza ipasavyo jengo hilo ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
No comments:
Post a Comment