Habari za Punde

Hutuba ya Bajeti ya Matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Yapitishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Wakati wa Mkutano wa Asubuhi leo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Makatibu wa Baraza wakipitisha Vifungu vya Matumizi na Mapato kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/2019 vikipitishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar, likipitisha Vifungu vya Matumizi na Mapato vya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora.kwa mwaka wa Fedha wa 2018/2019.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Mawaziri wakipitia makabrasha ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wakipitisha vifungu vya matumizi na mapato vya Wizara hiyo wakati wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi la Bajeti ya Fedha kwa Mwaka 2018/2019. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakipitia Vifungu vya Matumizi vya Bajeti ya Wizara hiyo wakati wa kupitisha Hutuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Mhe. Abdallah Maulid Diwanbi akitaka ufafanuzi wa Kifungu cha Matumizi cha Wizara hiyo wakati wa kupitisha Hutuba ya Bajeti ya fedha kwa mwaka 2018/2019 ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakipitia Vifungu vya Matumizi vya Bajeti ya Wizara hiyo wakati wa kupitisha Hutuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwatambulisha Wageni wa Waheshimiwa waliofika katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi kujionea uendeshaji wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.